Simba wameamua kuonyesha
ujasiri na kwamba wamepania kukisuka kikosi chao baada ya kuialika AS Vita de Kinshasa ya DR Congo.
Timu hiyo ndiyo imekuwa
ikiisumbua sana TP Mazembe kwenye ligi ya DR Congo na Ligi ya Mabingwa Ulaya na
sasa itacheza na Simba keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo inatarajia
kuwasili nchini kesho lakini imeelezwa kwa mafungu kwa kuwa wachezaji wake nane
wako timu ya taifa ya DR Congo inayocheza leo.
“Wao watawasili tofauti na
juhudi za kupata tiketi za ndege zinaendelea.
“Kweli ni timu ngumu na
kali, lakini sisi tumeamua kupata timu sahihi kwa ajili ya kujipima.
“Kujipima na timu laini ni
kujidanganya, hivyo tunaamini timu kama Gor Mahia halafu sasa tunapanda kwa AS
Vita ni sahihi zaidi,” alisema Mohammed Kigoma, mmoja wa viongozi wa kundi la
Friends of Simba (Fos).
0 COMMENTS:
Post a Comment