Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari zikielezea
tuhuma za hujuma kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za kufuzu
mashindano ya AFCON.
TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa
tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya. Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania litateua jopo la kuchunguza tuhuma hizi.
Wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania
(Members of TFF Family) watakaohitajika kuhojiwa na jopo hilo kwa mujibu wa
Ibara ya 37 ya Kanuni za Maadili za TFF watalazimika kutoa ushirikiano.
Atakayeshindwa kutoa ushirikiano atachukuliwa hatua za kimaadili.
Pia wadau wa mpira wa miguu ambao sio
wanafamilia wa TFF, watakaoitwa na jopo hili wanaombwa watoe ushirikiano kwa
nia ya kujenga mpira wetu.








0 COMMENTS:
Post a Comment