BARUA YA TFF KWENDA BODI YA LIGI AMBAYO INAONYESHA TFF SASA IMEGEUKIA HADI FEDHA ZA UDHAMINI ZA KLABU IKITAKA NAZO ZIKATWE. |
Uongozi wa TFF umeandika barua kwenye bodi ya ligi ukitaka ulipwe 5% ya fedha za udhamini kutoka Vodacom na Azam TV ipewe yenyewe.
TFF imetaka fedha hizo ili izitumie kwa ajili ya maendeleo ya soka au timu ya taifa.
Lakini hali imezishitua baadhi ya klabu ambazo zimeanza kuhoji chinichini kuhusiana na suala hilo.
Suala hilo la kushangaza kama litapita litakuwa ni la aina yake kwa klabu kutoa fedha zao za udhamini na kulipa shirikisho.
Suala hilo ambalo limeonekana litakuwa la kwanza kufanyika katika ulimwengu wa soka, bado haijajulikana kama limepitishwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment