YONDANI. |
Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, ametamba
kuwa yeye ni bora na anataka kulithibitisha hilo atakapokutana na Emmanuel Okwi
wa Simba katika mechi baina ya timu hizo, Oktoba 12, mwaka huu.
Yondani amesema hakuna ubishi yeye ndiye beki
bora kwa hivi sasa, hivyo anaamini hakuna mshambuliaji yeyote atakayemsumbua
ndani ya uwanja, akiwemo Okwi ambaye anazungumzwa zaidi katika kikosi cha
Simba.
Beki huyo ambaye wiki mbili zilizopita
alimdhibiti vizuri mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu katika mechi ya Ngao
ya Jamii, amekuwa akishirikiana vizuri na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye idara
ya ulinzi kwa miaka kadhaa tangu alipotua akitokea Simba.
“Nilianza na Kavumbagu aliyekuwa anatamba sana
kuwa atatufunga, sasa hivi nguvu na akili zangu nazielekeza kwa Okwi ambaye
naye anatamba kwamba atatufunga, ngoja tuone,” alisema Yondani.
0 COMMENTS:
Post a Comment