November 4, 2014


Hatimaye beki wa Azam FC, Erasto Nyoni amepatikana na uongozi wa klabu hiyo umethibitisha.

Jana jioni, Nyoni ambaye ni beki wa pembeni wa Azam FC na Taifa Stars alikutana na masaibu makubwa ya kupigwa vibaya kama mwizi na kundi la madereva bodaboda.
Nyoni hakuwa amejulikana yuko wapi hadi leo asubuhi, mtu mmoja alipowasiliana na daktari wa Azam FC.
“Kweli tuna mtu amewasiliana nasi na kutueleza Nyoni yu mzima,” alisema Meneja wa Azam FC, Jemedari Said.
Hadi jana usiku saa 4, Jemedari alikuwa akihaha kumtafuta Nyoni na alifika katika kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ lilipokuwa gari lake aina ya Toyota GX 110 likiwa limehifadhiwa.
Kutokana na kutojulikana yu wapi, hali hiyo ilisababisha hofu, hadi leo asubuhi ilipojulikana kuwa yupo salama.
Hali hiyo ilimtokea wakati alipoigonga bodaboda katika eneo la Manzese Tip Top jijini Dar es Salaam, akalazimika kukimbia kutokana na lundo la madereva hao kutaka kumvamia na kumpiga.
Lakini baadaye walimshika kwenye eneo la Kijitonyama na kumpiga kama mwizi, hali iliyomlazimu kuliacha gari lake na kutimua mbio.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic