December 1, 2014



Nahodha na beki wa kati wa Simba, Mganda, Joseph Owino, amepatwa na msiba wa dada yake ambao utamfanya achelewe kujiunga na Simba lakini mchezaji mwingine Mganda wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, naye pia ameomba kuendelea kubaki Uganda mpaka hapo atakapomaliza matatizo yanayomuandama.


Okwi na Owino ndiyo wachezaji pekee wa kimataifa wa Simba ambao mpaka sasa hawajajiunga na kikosi cha timu hiyo tangu walipoenda mapumzikoni nchini mwao mapema mwezi Novemba lakini wengine waliobakia ambao ni Warundi, Pierre Kwizera na Amissi Tambwe tayari wameshatua nchini tangu Jumatano iliyopita.

Mratibu wa safari za wachezaji wa kimataifa klabuni hapo, Salim Swaka, alisema kuwa wachezaji hao walipaswa kutua nchini kati jana au leo Jumatatu lakini sasa haitawezekana baada ya kupata udhuru ambapo kila mmoja akiwa na matatizo yake tofauti.

Alisema kwamba Owino amefiwa na dada yake ambaye alikuwa akimuuguza, hivyo ameomba kuongezewa siku zaidi kwa ajili ya kumaliza taratibu zote za mazishi kisha ndiyo atajiunga na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Mtani Jembe dhidi ya Yanga utakaopigwa Desemba 13, mwaka huu.



 “Mara ya kwanza walitakiwa kuja ndani ya siku mbili hizi yaani jana (juzi Jumamosi) na leo (jana Jumapili) lakini baada ya kutoa udhuru wao huo kwa hiyo sasa tunawategemea kutua nchini kuanzia katikati ya wiki hii,” alisema Swaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic