HANS POPPE. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zacharia Hans Poppe amesema baba wa kiungo wa Yanga, Simon Msuva
anapaswa kukaa kando katika suala la mwanaye.
Hans Poppe ambaye yuko nchini
Ujerumani, amesema mzazi huyo anapaswa kukaa kimya na kuwaacha Simba wamalizane
na Yanga na mwanaye.
MSUVA AKISHANGILIA NA WENZAKE BAADA YA KUIFUNGUA YANGA BAO. |
“Baada ya hapo yeye atampelekea dau
baba yake halafu atafurahia.
“Sidhani kama kuna mzazi anaweza
kumzuia mwanaye asipate fedha,” alisema Hans Poppe.
Kuhusiana na suala la kupeleka barua
ya kumtaka Msuva, Hans Poppe alisema wataipeleka mara baada ya kufunguliwa kwa
dirisha dogo.
Lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Beno
Njovu yeye alisema bado hawajapokea barua hiyo ya Simba.
“Hadi sasa hatujaona barua yoyote
kuhusiana na Msuva,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment