KIBADENI WAKATI AKIINOA SIMBA... |
Kocha wa zamani wa Simba na Kagera
Sufar, Abdallah Kibadeni amesema atafungua shule ya michezo itakayojumuisha ile
ya kikapu na netiboli.
Kibadeni amesema atafungua akademi
hiyo katika eneo la Chanika jijini Dar es Salaam na mchezo utakaoanza
kufundishwa ni soka.
“Soka ni namba moja ndugu yangu kwa
kuwa mimi ni mwalimu wa mchezo huo. Lakini kadiri siku zinavyosonga mbele,
tutafungua na michezo mingine.
“Mfano netiboli, kikapu. Hii ni
kuifanya kuwa shule ya michezo yote ile ambayo inaweza kutoa vijana na
kuendeleza vipaji vyao,” alisema.
Kibadeni alipoulizwa kuhusiana na suala
la kufundisha timu za Ligi Kuu Bara, alisema.
“Kwa kweli acha nipumzike, presha ni
kubwa. Watu hawaridhiki hata kidogo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment