Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesisitiza
kuwa kinda James Msuva ana nafasi ya kufanya vizuri.
James anayekipiga Simba B ni mdogo wa kiungo wa Yanga, Simon Msuva. Tayari Phiri alishasema anaona anaweza kumpandisha kikosi kikubwa.
Phiri amekumbushia namna alivyopandisha Haruna
Chanongo wakati akionekana ni kinda na kusema: “Hata huyu Msuva ana kitu
nakiona.”
Phiri amesema kiungo huyo ana vitu ambavyo
vinaweza kumfanya ang’are hasa kama atakuwa anaamini anaweza kufanya hivyo.
“Ninaendelea kumuangalia kama nilivyosema
awali, pia nitamuangalia katika mechi.
“Ni mchezaji ana vitu ambavyo kocha
anavihitaji, lakini lazima uwe mvumilivu.
“Tayari nimezungumza naye na kumueleza kwamba
lazima ajitume, awe na nidhamu na aweke malengo,” alisema Phiri.
Msuva yuko katika kikosi B na amekuwa akifanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Mwenge Shooting jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment