Uongozi wa timu ya Mgambo JKT, umesema
upo tayari kumuachia kiungo Sabry Makame anayewindwa na Yanga, wakati huu wa
usajili wa dirisha dogo.
Yanga inataka kumsajili kiungo huyo
ili kuimarisha nguvu katika safu yake ya kiungo baada ya kumkosa Jonas Mkude
aliyejipiga kitanzi cha miaka miwili Simba.
Kocha
wa Mgambo JKT, Bakari Shime, amesema wao hawana kipingamizi kwa mchezaji huyo kuondoka kwenda timu yoyote ile itakayofuata taratibu
na kufikia makubaliano.
Alisema wao ni timu ambayo inakuza
vipaji vya wachezaji na baada ya hapo timu nyingine zikitaka kuwasajili
wanawaruhusu ili kuendeleza vipaji vyao.
“Sisi ni kama akademi ya kukuza vipaji
vya wachezaji na baada ya kuonyesha kiwango kizuri tunawaruhusu kwenda kucheza
timu yoyote inayowahitaji na kuendeleza vipaji,” alisema Shime.
0 COMMENTS:
Post a Comment