November 17, 2014

RUVU SHOOTING.
PIGO! Kikosi cha maafande wa Ruvu Shooting, kimepata pigo la aina yake baada ya kuondokewa na mastaa wake saba ambao wanatakiwa kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi yatakayochukua takribani mwaka mzima.

Kuondoka kwa nyota hao kumeifanya timu hiyo kuingia sokoni katika dirisha hili dogo la usajili, ambalo lilifunguliwa juzi Jumamosi huku likitarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu.
Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire, amesema kutokana na kuondoka kwa nyota wao, kocha Tom Olaba amebainisha kwenye ripoti yake kuhitaji mastraika wawili.
“Kwenye ripoti ya mwalimu, amebainisha kuhitaji mastraika wawili katika dirisha hili la usajili. 

Lakini hii imetokana na wachezaji wetu kama watano mpaka saba wanatakiwa kuondoka kwenda mafunzoni na tutawakosa kama mwaka mzima,” alisema Bwire ambaye aligoma kuwataja wachezaji hao wanaotarajiwa kuondoka kwa kuwa hayo ni mambo ya kijeshi.

Ruvu ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi saba, ambapo imefanikiwa kushinda mechi mbili na sare moja katika michezo saba iliyocheza mpaka sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic