Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba,
Paul Kiongera, raia wa Kenya, amelazimika kuchelewa kupelekwa India kufanyiwa
matibabu ya goti kufuatia kuwepo kwa sherehe za wiki ya Kiislamu inayojulikana
kama Ashura.
Kiongera aliumia goti katika mchezo wa
kwanza wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambapo katika mchezo huo timu hizo
zilitoka sare ya 2-2.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema Kiongera alitakiwa kuondoka nchini wiki
iliyopita, lakini amecheleweshwa na sherehe za Kiisalamu ambapo nchini India
wamekuwa katika pilikapilika hizo na kudai kuwa daktari aliyepewa jukumu hilo,
ametaka apelekwe sherehe zitakapomalizika.
“Mikakati ya kumpeleka Kiongera bado
ipo palepale, kwani taratibu zote zimeshafanywa na bajeti ambayo tumeipanga ni
kuanzia Sh milioni 8.5 hadi 10, kwa ajili ya zoezi lote la kufanyiwa upasuaji.
“Alitakiwa aondoke nchini wiki hii
lakini imeshindikana kufuatia uwepo wa sherehe za wiki ya Kiislamu ambapo
daktari wake ametaka apelekwe mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo na
hatujajua atakaa muda gani huko,” alisema Aveva.
0 COMMENTS:
Post a Comment