Taswira ya picha tatu katika tukio lililotokea hivi karibuni kwa mchezaji wa Azam FC na timu ya taifa, Taifa Stars, Erasto Nyoni kupigwa vibaya kama mwizi na madereva bodaboda.
Nyoni alipigwa baada ya kumgonga dereva bodaboda, lakini alipotaka kushuka, wakaanza kumkimbiza hadi walipofanikiwa kumpata katika eneo la Kijitonyama ambako walimshambulia vibaya.
Picha zinaonyesha baadhi ya watu waliokuwa katika eneo la tukio wakionyesha fulana ya beki huyo ambaye alilazimika kuacha baada ya kushambuliwa vibaya na lundo la watu zaidi ya 30.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment