December 1, 2014

 
NYAMLANI (MWENYE SHATI LA MAUA) AKIWAVISHA MEDALI MABINGWA WA NDONDO CUP, ABAJALO FC HUKU AKISAIDIWA NA KOCHA WA MWADUI FC, JAMHURI KIHWELO 'JULIO'.
Mabingwa wa Ndondo Cup ni Abajalo FC ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Abajalo maarufu kama Mnyama Mkubwa ilibeba ubingwa huo jana baada ya kuifunga Tabata kwa mabao 7-6 ya miwaju ya penalti.



Kwa ubingwa huo, Abajalo ilibeba kitita cha Sh milioni 5 pamoja na kombe, wakati Tegeta waliondoka na Sh milioni 3.

Tabata walianza kupata bao kupitia Jerry Tegete kwa mkwaju wa penalti, lakini Abajalo ikasawazisha kupitia Rashid Ismail Mkoko aliyeingia kipindi cha pili.

Baada ya dakika za kawaida kwisha, ndipo mikwaju kwenye Uwanja wa Bandari jijini Dar, ikaanza.
Watu kibao walijitokeza wakiwemo wadau mbalimbali wa soka nchini.


Makamu wa Rais wa TFF wa zamani, Athumani Nyamlani ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo iliyoandaliwa na Clouds FM chini ya kipindi chake cha michezo cha Sports Extra chini ya uogozi wa Shaffi Dauda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic