Kikosi
cha Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini leo (Desemba 1 mwaka huu)
Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi
itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa
chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi
Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya
mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji
walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally Mohamed
(White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele Green
(Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African Lyon).
Gadiel
Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba), Hassan
Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed Simbaulanga
(African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa Sugar).
Miraji
Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Omari
Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Said
Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza Ramadhan (Mtibwa
Sugar).
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya
Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi ya
Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.
0 COMMENTS:
Post a Comment