December 13, 2014


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kuwa ulinzi umeimarishwa katika mchezo wa leo wa Nani Mtani Jembe 2 utakaozikutanisha timu za Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Simba na Yanga zitakutana kwa mara ya pili kwenye mchezo huo wa Mtani Jembe huku mashabiki wa Yanga wakikumbuka kipigo kutoka kwa Simba cha mabao 3-1.

Kaimu Mkurugenzi wa TFF, Martin Chacha, alisema mashabiki wasiwe na wasiwasi kuhusu usalama kwani wameandaa askari 400 wa kawaida na wa Kikosi cha Mbwa.


“Kwa upande wa usalama, tayari tumejikamilisha na mashabiki wasiwe na wasiwasi kuhusu jambo hilo kwani tumeandaa askari wa kutosha, pia hatutaruhusu mashabiki kuingia wakiwa na chupa za maji kwani wanaweza kuzitumia kama silaha,” alisema Chacha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic