December 10, 2014


Beki David Owino amesema anakwenda kufanya majaribio nchini Cyprus.


Rafiki wa karibu wa Owino, amesema rafiki yake huyo ameshindwa kuwaambia Simba ukweli uliosababisha aje kufanya majaribio.

"Owino hataki kusema ukweli, ana ofa ya kufanya majaribio Cyprus. Amekuwa akifanya mazoezi kwa ajili hiyo," alieleza rafiki yake huyo kutoka Nairobi.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema Owino angewasili leo mchana na tatizo kubwa lilikuwa ni suala la ndege kujaa.

Lakini rafiki wa Owino amesema beki huyo maarufu kama Calabar, ameona ni vema kwenda Cyprus kujaribu bahati yake.

"Nafikiri ataondoka hapa Nairobi baada ya siku chache kwenda Cyprus kwa majaribio," alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic