December 10, 2014


Baada ya kuzingua vya kutosha, hatimaye nahodha wa Simba, Joseph Owino ameungana na mwenzake.

Owino ameungana na Simba na kufanya mazoezi na wenzake leo jioni kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Simba imefanya mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Amaan kuanzia saa 10 hadi 12:30 jioni.

Owino alikuwa kati ya waliofanya mazoezi na kusaidia kushusha presha ya Wanasimba kabla ya mechi ya Bonanza la Nani Mtani Jembe, Jumamosi.

Ilielezwa Owino alifiwa na dada yake, akalazimika kusafiri kwenye Nairobi, Kenya kwa ajili ya mazishi.


Hata hivyo alizidisha siku alizokuwa amepewa kwa ajili ya kurejea. Taarifa zinaeleza alipewa siku nne, lakini amerejea baada ya siku sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic