December 1, 2014

CHUJI

Kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’, ametamba kuwa, uwezo wake kamwe hauwezi kuulinganisha na wa kiungo mpya wa timu hiyo, Mbrazili, Emerson Roque.

Emerson tayari yuko jijini Dar es Salaam na ameanza mazoezi na Yanga.
Chuji aliachwa na Yanga katika usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara baada ya mkataba wake kumalizika kabla ya kwenda Oman kwenye majaribio na kurejea nchini kwa kile kilichoelezwa kushindwa, akiwa na Betram Mwombeki na Mkenya, Jerry Santo.
EMERSON.

Chuji anayekipiga Mwadui FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, amesema yeye ni jembe.
 “Mimi aina yangu ya uchezaji kamwe hauwezi kuifananisha na huyo kiungo mpya wa Yanga, Emerson. Aina yangu mimi ya uchezaji inafanana na Renny (Ramadhani), katika hilo hakuna ubishi, muulize mchezaji yeyote aliyecheza soka zamani atakwambia tu.


“Na kama unabisha subiria ligi kuu ianze muone wenyewe, Chuji nitaendelea kuwa bora kila siku, kikubwa ninachowaambia mashabiki wangu wasubiri ujio wangu mpya nikiwa na Mwadui, ninataka kurejea kivingine kabisa katika kuhakikisha ninarejesha heshima yangu iliyopotea,” alisema Chuji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic