December 10, 2014

SSERUNKUMA (KUSHOTO)

Mshambuliaji mpya wa Simba, Danny Sserunkuma, amesema pamoja na ugeni wake nchini, lakini ana imani atacheza vizuri katika mechi dhidi ya Yanga, Jumamosi.

Sserunkuma raia wa Uganda aliyesajiliwa na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya, amesema mchezaji anapoingia uwanjani ana uwezo wa kuzoea mambo haraka.

“Naweza kuzoea haraka, lakini ni jambo la kujifunza kwa kuwa soka la Tanzania linaweza kuwa na mambo machache tofauti na Kenya.

“Lakini kwa mchezaji, lazima uwe tayari kila wakati. Najua wengi watakuwa wageni, hatujazoeana, lakini tutaweza tu kucheza kama timu kwa kuwa tumeanza mazoezi ya pamoja hapa Zanzibar,” alisema.


Sserunkuma yupo kambini Zanzibar ambako kikosi cha Simba kinajifua kujiandaa na mechi hiyo ya Bonanza la Nani Mtani Jembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic