December 1, 2014

MGAMBIA WA SIMBA AKIJIFUA...
Simba imeshusha kifaa kingine kwa ajili ya majaribio, mambo yakiwa safi, kinaanguka saini.


Huyo ni mshambuliaji huyo, Omar Mboob aliyewasili juzi usiku kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Leo asubuhi, Mboob ameanza mazoezi na kikosi cha Simba kwenye gym ya Chang'ombe.

Baada ya hapo akaungana nao kwenda kwenye Uwanja TCC Chang'ombe jijini Dar.

SALEHJEMBE baadaye ilimshuhudia mshambuliaji huyo akishushwa kwenye hoteli ya kisasa ya Sapphire Court ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, juhudi za kutaka kuzungumza naye zilikwama baada ya kuingia ndani ya hoteli na walinzi kuonekana ni wakali wakitaka asibugudhiwe.

Taaifa zinaeleza wakala kutoka Ufaransa ndiye amemleta nchini na uongozi wa Simba umethibitisha kwamba amekuja kwa majaribio.

Iwapo atafanikiwa, inaonekana Amissi Tambwe au Paul Kwizera, mmoja wapo ataonyeshwa mlango wa kutokea.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic