December 1, 2014


Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Manuel Neuer ndiyo vichwa vitatu vilivyoteuliwa kuwania tuzo ya FIFA Ballon d'Or 2014.

Watatu hao ndiyo wameingia fainali na mshindi atapatikana Januari 12, 2015.

Neuer, 28, aliteuliwa mara ya mwisho mwaka 2006 kuwania tuzo hiyo, usisahau ndiye aliiwezesha Ujerumani kubeba Kombe la Dunia Brazil mwaka huu.


Messi, ndiye mchezaji anaongoza kwa kutwaa tuzo nyingi kama hizo, amebeba mara nne na kwa jina la Ballon d'Or ni kwa miaka hii (2009-2012).

Cristiano Ronaldo anapambana kupata tuzo yake ya tatu Ballon d'Or.

Alitwaa ya kwanza mwaka 2008 akiwa na Manchester United na mara ya mwisho akiwa na Real Madrid na ndiye mtetezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic