January 19, 2015



Chama cha Wanasoka Tanzania (Sputanza) kimelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuchukua hatua kwa beki wa Ruvu Shooting, George Michael kutokana na kitendo chake cha kumkaba mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe.

KISOKI...

Tambwe ameonekana akikabwa na beki George Michael wa Ruvu Shooting.

Picha hiyo iliyozua gumzo imechapishwa katika Gazeti namba moja nchi la michezo la CHAMPIONI.

Kisoki ameiambia SALEHJEMBE kwamba picha ile inapoteza uungwana wa michezo uwanjani.

"Ule si uungwana, mchezo wa soka si kuumizana. Soka ni kushindana na kama mkitokea kuumizana inakuwa ni bahati mbaya mnaombana msamaha.

"Sasa ile ya Tambwe na yule beki si jambo jema, mtu anamkaba mtu utafikiri anataka amtoe roho," alisema Kisoki.

TFF wabaweza kulifanyia kazi suala hili na ikiwezekana wachukue hatua mara moja, sisi tunataka soka la kiungwana.




2 COMMENTS:

  1. Sidhani kama kuna hatua yoyote itachukuliwa,ngoja tususbiri.

    ReplyDelete
  2. Haikuwa mechi ya amani kwa kweli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic