Mzunguko
wa pili wa Ligi Daraja la Pili (SDL) sasa utaanza Januari 31 mwaka huu, badala
ya Januari 24 mwaka huu kama ilivyopangwa awali ili kutoa fursa kwa Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kupitia usajili wa dirisha dogo.
Timu
zinazocheza ligi hiyo katika makundi manne tofauti ni; Milambo FC, Mji Mkuu FC
(CDA), Mvuvumwa FC, Singida United, na Ujenzi Rukwa (Kundi A), Arusha FC, Bulyanhulu
FC, JKT Rwamkoma FC, Mbao FC, na Pamba SC (Kundi B).
Nyingine
ni Abajalo FC, Cosmopolitan, Kariakoo Lindi, Kiluvya United, Mshikamano FC, na
Transit Camp (Kundi C), wakati Kundi D ni Magereza Iringa, Mji Njombe, Mkamba
Rangers, Town Small Boys, Volcano FC, na Wenda FC
0 COMMENTS:
Post a Comment