January 20, 2015


Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane amerudi darasani na Mei, mwaka huu atahitimu.


Zidane aliondolewa kwenye kikosi cha wakubwa cha Real Madrid kutokana na kutokuwa na vyeti vinavyomruhusu kukaa kwenye benchi la timu inayocheza La Liga na michuano ya Ulaya.

"Kweli naweza kusema hilo limeisha, niko darasani sasa. Mei, mwaka huu nitamaliza. Baada ya hapo nitaendelea na kazi yangu ya kufundisha.

"Napenda sana kufundisha, lakini hili lilikuwa lazima lifanyike, utaona nakaribia kumaliza," alisema.

Kuhusiana na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Zidane amesema mshambuliaji huyo ana nafasi ya kushinda tena tuzo ya Ballond'Or.

"Kwa hali ilivyo, hakuna cha kumzuia Ronaldo kushinda tena tuzo hiyo. Ninaamini atafanya hivyo kwa mara nyingine tena," alisema Zidane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic