January 19, 2015



Pamoja na tukio la mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga kukabwa kikatili na beki katili George Michael wa Ruvu Shooting, msemaji Masau Bwire ametoa kejeli bila ya huruma.


Masau amesema Yanga walidhani wanauza mayai kwamba wasiguswe huku akiwa na hofu picha hiyo iliyochapishwa leo na gazeti maarufu la michezo la CHAMPIONI imetengenezwa.
MASAU
"Sasa wenyewe waliona kama wanauza mayai, kwamba wakiguswa yataanguka. Ule ni mchezo wa kiume na kukabwa ni kawaida tu.
"Sioni kama kuna sababu ya kulalamika, hata wao yanga waliwaumiza wachezaji wetu, lakini mbona haijaonyeshwa.

"Siku hizi kuna teknolojia ya kila aina, huenda hata zile picha zimetengenezwa," alisema Masau.

Picha hiyo ya CHAMPIONI imekuwa gumzo kubwa ikimuonyesha Michael akimkaba Tambwe huku damu zikimtoka mdomoni.

Tambwe alisema beki huyo alimkaba na kumpiga vibao mara kwa mara.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic