Moussa Sow aliyeingia kipindi cha pili ameifungia
Senegal bao la pili katika dakika za majeruhi na kuiwezesha kupata ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Ghana.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa timu hizo hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika inayofanyika nchini Equatorial Guinea.
Ushindi huo ni muhimu kwa Senegal ambayo ipo kundi C maarufu kama kundi la kifo kwa kuwa timu nyingine ni Algeria na Afrika Kusini.
Ushindi huo ni muhimu kwa Senegal ambayo ipo kundi C maarufu kama kundi la kifo kwa kuwa timu nyingine ni Algeria na Afrika Kusini.
Ghana ilitangulia kupata bao kwa mkwaju wa penalti
kupitia Andre Ayew. Lakini Senegal wakasawazisha.
Kipindi cha pili kilikuwa na ushindani mkubwa na
Simba hao wa Milima ya Terranga walifanikiwa kupata bao zikiwa zimebaki sekunde
kumi kabla ya mpira kwisha baada ya dakika tatu kuwa zimeongezwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment