Mshambuliaji mpya wa Simba, Danny Sserunkuma amesema anaanza kujisikia yuko nyumbani hali itakayomsaidia kufanya kazi yake vizuri.
Sserunkuma amesema kuanzia wiki mbili zilizopita, ameanza kuzoea vizuri mazingira ya Tanzania.
"Sasa naanza kuona niko nyumbani, kubadili mazingira kawaida si kitu lahisi. Sasa naweza kufanya mambo yangu vizuri," alisema.
Aidha, Sserunkuma raia wa Uganda aliyejiunga na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya aliwashukuru wachezaji na viongozi wa Simba kwa ushirikiano unaomfanya aone sasa yuko nyumbani.
Tayari Sserunkuma ameifungia Simba bao moja katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara alizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment