Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
imewapiga faini na kuwafungia mechi wachezaji wawili wa Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa kufanya vitendo kinyume na kanuni
zinazotawala ligi hizo.
Mshambuliaji Haruna Chanongo wa
Stand United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga
teke mwamuzi wa mechi dhidi ya Polisi Morogoro iliyochezwa Januari 3 mwaka huu
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni
ya 37(3) ya Ligi Kuu.
Kipa Amani Simba wa Oljoro JKT
amepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kukataa kupeana mkono na viongozi wakati wa
kusalimia kabla ya kuanza mechi kati ya timu yake na Toto Africans iliyofanyika
jijini Mwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14 ya FDL.
Timu ya Polisi Mara imepigwa
faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa mechi ya
FDL dhidi ya Mwadui ya Shinyanga iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
mjini Musoma. Pia Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na
vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 40 dhidi ya Geita Gold, adhabu
ambazo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 41.
Na yule askari aliyemkwida Tambwe achukuliwe hatua.
ReplyDelete