Glavu alizovaa Muhammad Ali na Sonny Liston
wakati wakipambana mwaka 1965 zimeuzwa kwa kiasi cha pauni 622,000 (zaidi ya Sh
bilioni 1.5).
Glavu hizo alizivaa Ali wakati akimshinda Liston
katika pambano kali lililobaki kuwa gumzo.
Pambano hilo lilifanyika Mei 25 kwenye Ukumbi wa
American City of Lewiston, Maine nchini Marekani.
Licha ya mabondia hao kuwa na upinzani mkali na
pambano hilo kuzungumzwa kwa kipindi kirefu, Ali alishinda kwa KO katika raundi
ya kwanza.
Ngumi iliyomaliza pambano hilo katika raundi ya
kwanza ilipewa jina la 'phantom punch' na hadi sasa ndiyo ngumi maarufu zaidi
katika mchezo wa ngumi duniani.
0 COMMENTS:
Post a Comment