KIKOSI CHA VILLA SQUAD |
Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa
Squad, Mbarouk Kassanda kwa kusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao
haukufuata kanuni za usajili.
Villa
Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala
ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad
ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki
ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko
ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad
kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni
mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati
ilimuita mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa
kubadili majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili
lilibaki kuwa suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati
haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya
mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda
ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu
hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment