Rais wa
Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salama za
pongezi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer), Bw. Ahmed
Mgoyi kwa ushindi wa jumla wa mabao 12- 9 dhidi ya timu ya Taifa kutoka nchini
Kenya.
Timu ya Taifa
ya Tanzania ya Sola la Ufukweni, mwishoni mwa wiki iliibuka na ushindi wa mabao
7-6 katika mchezo uliofanyika kwenye Ufukwe wa klabu ya Escape 1 eneo la
Msasani Jijini Dar es Salaam.
Katika salamu
zake Malinzi amesema ushindi walioupata timu ya soka la Ufukweni mwishoni
mwa wiki, umeitangaza vizuri nchi ya Tanzania na kuwataka Viongozi wa soka la
Ufukweni, makocha, wachezaji kutobweteka na ushndi huo, zaidi kujipanga kwa
maandalizi ya mchezo utakaofuata.
Baada ya
kuitoa timu ya Taifa ya Kenya, Tanzania watacheza na timu ya Taifa ya Misri
mapema mwezi ujao ambapo mchezo wa awali utafanyika jijini Dar es salaam kati
ya mwezi Machi 7, 8 na marudiano kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.
Endapo timu
ya Taifa ya Tanzania itaiondoa timu ya Taifa ya Misri, moja kwa moja itakata
tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa Soka la Ufukweni 2015
zinazotarajiwa kufanyika Visiwa vya Shelisheli kuanzia April 14 - 19 mwaka huu.
Kwa niaba ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni kwa
ushindi huo na kuwatakia maandalizi mema kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya
Misri.
0 COMMENTS:
Post a Comment