February 12, 2015


Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema watakuwa wakichanganya mazoezi yao katika viwanja vya Karume na Taifa jijini Dar.


Yanga imeanza rasmi kujiwinda kwa ajili ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya Botswana itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Pluijm amesema wameamua kufanya hivyo kwa malengo tofauti kwa kuwa Taifa ndiyo watakaochezea mechi dhidi ya Waswana nao lakini Karume itawasaidia kumiliki mpira.

“Eneo la kuchezea na Karume ni bora zaidi, tukicheza pale ni lahisi wachezaji kupata mazoezi ya kutosha hasa katika suala la kumiliki mpira.

“Unapocheza nyumbani, lakini uwe na uhakika wa kukaa na mpira muda mwingi. Hauwezi kushambulia kama hauna mpira.

“Nyumbani lazima ushinde, hivyo tumeanza kufanya mazoezi ya aina tofauti,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic