Kocha Amri Said 'Stam' ameanza kazi ya kuinoa Polisi Morogoro akitokea Mwadui FC ya Shinyanga.
Amri aliyewahi kukipiga Simba, anatarajia kuungana na Jamhuri Kihwelo 'Julio' ambaye bado anafanya mazungumzo na uongozi wa Polisi Morogoro. Wawili hao ndiyo walioipandisha Mwadui FC kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu.
Msemaji wa Polisi, Clement Bazo amekiri wako katika mazungumzo na Julio.
"Mazungumzo yanaendelea kwa kweli, bado hatujafikia mwafaka ila Amri Said tunaye na ameanza kazi. Sasa yuko na timu ikiwa njiani kwenda Mbeya," alisema Bazzo.
Polisi inafanya kila juhudi kuboresha benchi la ufundi kuhakikisha inabaki ligi kuu..







0 COMMENTS:
Post a Comment