Kopunovic raia wa Serbia amesema, mambo mengi waliyopanga na kujifunza mazoezini kulingana na alivyoiona Yanga, yalifanyika.
"Nidhamu ilikuwa juu, wachezaji walijua nini kinafuatia baada ya kitu fulani. Tulifanya mafunzo ya kutosha na ilionekana walifuata mambo mengi.
"Lakini walikuwa na juhidi na walionyesha wazi kuwa walitaka kushinda mchezo huo na hilo ndiyo jambo bora kabisa.
"Mategemeo ni kufanya vizuri zaidi baada ya hapo, nawapongeza wachezaji na mashabiki wa Simba. Tunaupongeza uongozi kwa kutuunga mkono na tumepania kufanya vizuri zaidi," alisema Kopunovic ambaye timu yake ilionyesha soka safi, hasa kipindi cha pili cha mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment