March 11, 2015




Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck amekuwa mkweli kuliko unavyotegemea baada ya kuweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa Manchester United.


Welbeck amekuwa wazi kwa kusema aliifunga Man United bao la pili katika robo fainali ya Kombe la FA na kuing’oa katika hatua ya robo fainali, lakini haikuwa kazi lahisi.

Welbeck ametua Arsenal akitokea Man United ambako alikuzwa kisoka kwenye academy ya klabu hiyo lakini Arsenal ikashinda 2-1 ndani ya Old Trafford yeye akiwa shujaa kwa kufunga bao la pili.
'Manchester United ni klabu niliyo na mapenzi nayo,” alisema Welbeck, aliyeitumikia United kwa miaka 15 tokea akiwa na miaka nane.
“Mimi shabiki wa United, haikuwa kazi lahisi kuwang’oa lakini nilikuwa nafanya kazi yangu.

“Lakini nionyeshe mimi ni professional, pia ninayelenga mafanikio,” alisisitiza.

Mashabiki wa Man United walimpokea Welbeck kwa heshima na kumshangilia wakati timu hizo zikipasha misuli ikiwa ni sehemu ya kuonyesha hawakufurahia uamuzi wa Kocha Louis van Gaal kumuuza.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic