| BANDA (KUSHOTO) AKIWA NA OWINO... |
Kocha Mkuu wa Simba,
Mserbia, Goran Kopunovic, ametamka kuwa mfumo wa kuanzisha viungo watatu katika
timu hiyo utaendelea kutumika kutokana na kuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi
chake.
Tangu kuwasili kwa kocha
huyo katika kikosi hicho, ameweza kukibadilisha katika mfumo wa kiuchezaji
kutoka ule wa 4-4-2 uliokuwa unatumiwa na Mzambia, Patrick Phiri mpaka 4-3-3
ambapo viungo Abdi Banda na Jonas Mkude wamekuwa wakicheza kama wakabaji huku
Said Ndemla akicheza kama mchezeshaji.
Kopunovic alisema ataendelea kutumia mfumo huo wa kuanzisha viungo
watatu katika mechi zao kutokana na kuwa na faida.
“Nitaendelea kutumia mfumo wa
4-3-3 katika michezo yetu kutokana na kuwa na faida kubwa kwa upande wetu kwa
sababu tunakuwa na uwezo wa kuwazuia wapinzani wetu kuanzia katikati ya uwanja.
“Vilevile mfumo huo
umeonekana kueleweka na wachezaji wameuzoea kwa haraka zaidi, hivyo hakuna
sababu yoyote ya kuachana nao kwani hata hivyo umetufikisha katika nafasi nzuri
kwenye msimamo wa ligi kuu,” alisema Kopunovic.







0 COMMENTS:
Post a Comment