March 13, 2015


Juhudi za Tanzania kufanya vizuri katika soka la ufukweni zimeanza kupotea baada ya kuchapwa kwa mabao 6-2 wakiwa nyumbani jijini  Dar es Salaam.


Misri ambao ni wazoefu wa michuano hiyo wameichapa Tanzania kwa mabao 6-2 katika mechi ya kwanza kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika iliyopigwa kwenye ufukwe wa Escape One jijini Dar.

Tanzania ndiyo ilianza kufunga mabao mawili huku ikionekana kama watoto hao wa Falao wamepotea.
Lakini walianza kurejesha bao moja baada ya jingine hadi yalipofikia sita.

Uzoefu mkubwa walionao katika mchezo huo ulionekana ni mzigo kwa vijana wa Tanzania ambao walionyesha juhudi ambazo hata hivyo hazikuzaa matunda.


Tanzania imekutana na Misri baada ya kuitoa Kenya kwa kuichapa nyumbani Dar na ugenini Mombasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic