Baraza la sanaa
Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya
Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki
yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika.
Mwisho mwa mwezi
wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki
mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya na kumtakia
kila laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya
vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika
Mkurugenzi
Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua
katika halfa fupi ya pongezi kwa Nalimi Mayunga katika ofisi za BASATA
alisema” Ushindi huu ni furaha kubwa kwetu sisi Baraza la Sanaa la
Tanzania kwani tunayo dhamana ya kuhakikisha tunaendeleza sanaa nchini
kwa tunashirikiana na wadau mbalimbali nchini katika kuwawezesha
vijana wenye vipaji kukuza sanaa zao ndani na nje ya nchi.
Nachukua fulsa
hii kwa niaba ya BASATA kumpongeza Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga kwa kufanya
vizuri na kushinda mashindano haya.
Nawashukuru sana
Airtel kwa kufata taratibu stahiki na kushirikisha BASATA tangu mashindano haya
yaanze ikiwa ni kusajili kampuni yao na kupata hati ya kufanya shughuli
za sanaa na pia kutushirikisha katika mchakato mzima wa mashindano haya na
kumleta mshindi huyu kuchukua hati maalumu ya kusafiri na kuagwa rasmi wakati
wa kuondoka kwenda kwenye mashindano ya Afrika.
Kwakweli huu ni mfano wa
kuigwa na wadau wengi na wasanii kwa ujumla, kufata taratibu na kupata vibali
maalumu pindi wanapoenda nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa na kuwakilsisha
nchi yetu.
"Natoa wito kwa
watanzania kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya msimu wa pili wa mashindano haya
ya Airtel Trace yatakapotangazwa ili nao waweze kupata nafasi ya kushiriki na
kuinua vipaji vyao," alisema Shalua.
Akizungumza kwa
niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando
alisema Tunawashukuru watanzania wote walioshiriki katika shindano
hili tangu tulipolizindua.
"Tunampongeza sana Mayunga kwa ushindi
huu. Nalimi Mayunga ameweza kujishindia dili la kwenda Marekani na kupata
mafunzo chini ya usimamizi wa Akon,na pia kuweza kurekodi wimbo na video yake
ya kwanza vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekai 500,000/=
Tunategemea baada ya mafunzo hayo na kutoa wimbo wake na Akon basi mayunga
ataendelea kufanya vizuri na hatimae kuweza kuzifikia ndoto zake," alisema.
Airtel
ilimkabithi Mayunga zawadi ya shilingi million 50 za kitanzania kufatia ushindi
wake hapa nchini na sasa anajiandaa kwenda marekani na kufanya kazi na
msaani nguli Akon.
Akiongelea
ushindi wake Mayunga alisema, nawashukuru sana watanzania kwa kunipigia kura
toka mashindano haya yaanze, najisikia furaha kupata nafasi hii ya pekee na
naamini safari yangu nchini marekani itakuwa ya mafanikio makubwa na mwanzo wa
mafanikio katika kuzifika ndoto zangu za kuwa mwanamuziki nyota ndani na nje ya
nchi.
Nawashukuru
Airtel kwa kuanzisha mashindano haya na BASATA kwa kunipa ushirikiano
wakati wote wa mashindano. Natoa wito kwa watanzania na vijana wenzangu
kuchangamkia fulsa hii pindi msimu wa pili wa mashindano haya yatakapotangazwa
na kuanza .
Mashindano ya Afrika
yalimalizika kwa mtanzania kushika nafasi ya kwanza , Nigeria nafasi ya
pili na Congo Brazavile nafasi ya tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment