Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesisitiza wataendelea
kupambana kupata nafasi ya pili.
Kuponovic raia wa Serbia amesema wana uwezo wa kupata nafasi ya
pili kama watashinda mechi tatu mfululizo.
“Inawezekana kabisa, kinachotakiwa sisi ni kushinda mechi zetu
tatu zinazokuja.
“Baada ya mechi hizo, litafuatia suala la kuangalia wapinzani wetu
Azam FC wanakwenda vipi.
“Kwa sasa kitu cha msingi kwetu ni kushinda mechi zetu tatu
mfululizo, halafu tunaweza kutulia na kuangalia hesabu upya.
“Morali ya wachezaji ipo juu, tunaamini tunaweza kufanya vizuri
zaidi,” alisema Kopunovic.
Simba iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 wakati Azam FC
imetoka sare ya bila kufungana na Mgambo Shooting leo na kufikisha pointi 39.
0 COMMENTS:
Post a Comment