ISIHAKA |
Nahodha wa kikosi cha timu
ya Simba, Hassan Isihaka, ametamka wazi kuwa ndoto zao kwa sasa ni kuona kikosi
hicho kinamaliza katika nafasi ya pili ili kuweza kujikatia tiketi ya kushiriki
mashindano ya kimataifa.
Mara ya mwisho kwa kikosi
hicho cha Simba kushiriki mashindano ya kimataifa ilikuwa misimu mitatu
iliyopita ambapo walitolewa na Clube Desportivo do Libolo FC ya Angola.
Isihaka amesema kwa sasa
wameelekeza nguvu zao katika kuhakikisha kikosi hicho kinamaliza katika nafasi
ya pili katika msimamo wa ligi ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki michuano
ya kimataifa ambapo kwa kipindi kirefu wamekuwa watazamaji.
“Kwa sasa tumejitolea
wachezaji wote kupigana kwa nguvu zetu katika kila mechi ili kupata matokeo
mazuri ambayo yatatusaidia katika harakati za kuweza kumaliza katika nafasi ya
pili kwenye msimamo wa ligi kuu.
“Tumepania kumaliza katika
nafasi hiyo ili kuweza kuirudisha tena timu katika mashindano ya kimataifa
ambayo kwa kipindi kirefu sasa tumekuwa watazamaji tukiwaacha wapinzani wetu
Yanga na Azam washiriki,” alisema beki huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment