Baada ya benchi ya ufundi la Kagera Sugar kufungashiwa virago hivi karibuni, aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrage Kabange, amefunguka kuwa anashukuru ameondoka salama ndani ya kikosi hicho na kwa sasa anafungua milango kwa timu yoyote ile.
Kabange alianza kukinoa kikosi hicho mwaka 2006 mpaka mwaka huu kama kocha msaidizi akiwa na makocha wakuu tofauti, ambapo mkataba wake umemalizika hivi karibuni.
Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo umefanya mabadiliko na tayari umemtangaza kocha mkuu Mbwana Makata huku ukiendelea kusaka kocha msaidizi.
Kocha huyo mkongwe amesema kuwa anashukuru amefanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa bila kugombana na uongozi wa klabu hiyo.
“Ni kweli nimemaliza mkataba na Kagera na nashukuru Mungu nimemaliza salama bila ugomvi na nimedumu zaidi ya miaka tisa, sasa ni wakati wa kuangalia maisha kwingine,” alisema Kabange.
0 COMMENTS:
Post a Comment