Msanii maarufu wa Kundi la Orijino Komedi, Joseph
Shamba ‘Vengu’, yupo mbioni kurudi mzigoni baada ya hali yake ya kiafya
kuendelea vizuri.
Kwa muda mrefu Vengu alikuwa haonekani katika
kundi hilo la vichekesho kutokana na kuugua kwa muda mrefu lakini hivi sasa
afya yake imedaiwa kuimarika.
Kaka wa Vengu,
Andrew Shamba ambaye pia ni Mwamuzi wa Ligi Kuu Bara, alisema kuwa mdogo wake
huyo anaendelea vizuri na muda wowote ataungana na wenzake.
“Tunamshukuru Mungu ndugu yetu anaendelea vizuri
kabisa na muda wowote ataungana na wenzake kuendelea na kazi yake ya vichekesho.
“Kwa sasa yupo nyumbani kwake Kigamboni
akiendelea na ratiba yake ya mazoezi ya kila siku ambayo alipewa baada ya
matibabu aliyofanyiwa nchini India,” alisema Shamba.
Aliongeza: “Kwa sasa haruhusiwi kuonekana
hadharani mpaka hapo muda wake wa mazoezi utakapokuwa umemalizika na hiyo ni
kutokana na kumuepusha na watu wanaoweza kumkumbusha mambo yaliopita ambayo
husikitisha sana na kumfanya awe na mawazo mengi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment