KISIGA (KUSHOTO) WAKATI AKIWA MTIBWA, HAPA AKIPAMBANA NA ATHUMANI IDD 'CHUJI'. |
Klabu ya Mtibwa Sugar imeweka wazi msimamo wake
kuwa ipo tayari kuwapokea wachezaji wake wote wa zamani ambao wanahitaji
kurejea klabuni hapo, isipokuwa Shabani Kisiga kutokana na kuwa na rekodi mbaya
ya nidhamu.
Kuna taarifa kuwa huenda wachezaji hao wakiwemo
Hussein Javu, Nizar Khalfan wa (Yanga), Hussein Sharif ‘Cassilas’, Issa Rashid
‘Baba Ubaya’ (Simba) wanaweza kurejea klabuni hapo.
Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru,
amesema hivi:
“Wachezaji wanapoondoka Mtibwa si tatizo, jambo
la msingi ni kufuata taratibu, ndiyo maana hatuwazuii kurejea lakini kwa Kisiga
siyo rahisi kupokelewa kutokana na kuwa na makosa ya mara kwa mara.”
Aidha, Kocha Mecky Maxime ameshakabidhi ripoti
yake klabuni hapo ambapo bodi itakutana Juni, mwaka huu kuijadili.
0 COMMENTS:
Post a Comment