Kiungo wa Simba, Jonas Mkude, amesema
amefurahishwa na kitendo cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa
Stars, lakini akasisitiza kuwa bado hajui sababu za yeye kutoitwa awali.
Kocha wa Stars, Mart Nooij, hakumuita Mkude
kikosini licha ya kuwa kwenye kiwango kizuri huku akigoma kutoa sababu na kudai
kuwa Mkude ni mchezaji mzuri kwa makocha wengine siyo yeye, lakini amemuita
kikosini katika kile kilichoonekana ni baada ya kupata presha kubwa kutoka kwa
wadau mbalimbali waliohoji.
“Kuitumikia timu ya taifa ni jambo zuri na
nimefurahi kwa kuwa uwezo ninao,” alisema Mkude.
Alipoulizwa kama ameambiwa sababu za kutoitwa
awali, alisema: “Bado sijajua sababu, naamini kocha ndiye anafaa kujibu hilo
swali, labda kuna kitu anaona kinapungua kwenye kikosi chake ndiyo maana
ameamua kuongezea nguvu nyingine.”
0 COMMENTS:
Post a Comment