Kocha wa zamani wa
Simba, Goran Kopunovic amesema iwapo Simba watafanikiwa kumnasa Laudit Mavugo,
atatoa msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji.
Akizungumza na
SALEHJEMBE, Kopunovic amesema Mavugo ni mmoja wa wachezaji wenye kiwango kizuri
katika ushambuliaji.
“Ni mshambuliaji mzuri,
ana kasi, nguvu, anapiga mashuti, pia mzuri wa mipira ya juu kutokana na mfumo
unaotumiwa na kocha.
“Ninaamini ataongeza
chachu ya Simba kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji,” alisema Kopunovic ambaye
ndiye alimpendekeza Mavugo raia wa Burundi.
Mavugo sasa ni
mshambuliaji tegemeo wa Vital’O ya Burundi. Pia timu ya taifa ya Burundi na
tayari yuko katika hatua nzuri ya mazungumzo na mshambuliaji huyo.
Kabla Mavugo aliwahi
kufanya kazi pamoja na Kopunovic katika kikosi cha Polisi Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment