May 17, 2015


Kocha wa Polokwane City, Kosta Papic ameshinda na kuwa kocha bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Papic aliyewahi kuinoa Yanga  ameshinda tuzo hiyo ya wasomaji wa jarida la soka la Kickoff .

Kocha wa Free State Stars, Kinnah Phiri ambaye sasa anakuwa kocha wa Mtanzania, Mrisho Ngassa naye alikuwa kati ya walioshirikishwa.

Papic raia wa Serbia amepata asilimia 38.1 baada ya kubeba kura 787 kati ya 2066.

Phiri amepata kura 135 akiwa amezidiwa na Steve Komphela aliyepata 370 na Rodger de Sa aliyechukua 449.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic