SINGWACHA |
Bondia Kiatchai
Singwancha tayari ametua jijini Dar es Salaam kumvaa Francis Cheka.
Cheka anapanda ulingoni
kupambana na Mthai huyo keshokutwa Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA jijini Dar es
Salaam.
Singwancha ameonekana
kujiamini na kusisitiza kwamba ana uhakika atafanya vizuri.
Mara baada ya kutua
kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), leo mchana, bondia huyo
alionekana kuwa kivutio kwa wengi kutokana na ukubwa wa umbo lake, maana ni
mrefu, mwembamba na anaonekana kuwa na mwili uliojengeka vema kimazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment