Hatimaye sasa
Azam FC nayo imeanza kutanua makucha na tayari imetua kwenye timu maarufu
Afrika, TP Mazembe ya DR Congo na kutaka saini za wachezaji wawili hatari wa
timu hiyo.
Taarifa makini
zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa mabosi wa ngazi ya juu Azam, zimebainisha
mpango huo wa kuwataka wachezaji hao raia wa DR Congo walio kwenye kikosi cha
kwanza cha Mazembe ambao mmojawao anamudu nafasi ya beki wa kulia na mwingine
ni straika.
Chanzo hicho
kimefafanua kuwa imekuwa ngumu kuwashawishi wachezaji hao na sasa wamemua
kumtumia mshambuliaji wa timu hiyo, Mtanzania, Mbwana Samatta ambaye alikubali
na ameonyesha kupata mafanikio makubwa katika kukamilisha zoezi hilo.
Taarifa zinaeleza
kwamba awali wachezaji hao ambao mpaka sasa majina yao bado ni siri, walikuwa
wagumu walipoelezwa suala la kuhama Congo na kuja kukipiga Tanzania lakini
baadaye baada ya kushirikishwa Samatta ambaye ni straika tegemeo wa timu hiyo,
sasa mambo yameanza kulainika na mchakato unakwenda vizuri.
“Kuna
wachezaji kwa sasa tunawatafuta kwa ajili ya kuweka mambo sawa msimu ujao na
kuzidi kusonga mbele zaidi ya hapa tulipo sasa, tayari kuna harakati za kumpata
beki mmoja wa kulia na mwingine ni straika, wote raia wa Congo.
“Wanacheza TP
Mazembe, tuliamua kumtumia Samatta kwa kuwa awali ilikuwa ngumu kuwapata,”
alisema bosi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, juu ya suala hilo alikana
na kusema: “Hakuna suala kama hilo.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment