KATIKA PICHA HII, WACHEZAJI WATATU TAYARI WAMEONDOKA. KUSHOTO NI NONGA, WATATU KULIA NI DEUS KASEKE NA WA KWANZA KULIA NI ANTHONY MATOGOLO. |
Imefahamika kuwa maslahi madogo yaliyopo kwenye Klabu ya Mbeya City ndiyo sababu kubwa ya
wachezaji nyota kuikimbia timu hiyo.
Mbeya City
ambayo imekuwa na jina kubwa ndani ya misimu miwili iliyocheza Ligi Kuu Bara,
imekimbiwa na wachezaji wanne waliokuwa katika kikosi cha kwanza ambao ni Peter
Mwalyanzi aliyetua Simba, Deus Kaseke (Yanga), Paul Nonga na Anthony Matogolo
(Mwadui FC).
Nonga ambaye
ametua Mwadui na kupewa mkataba wa mwaka mmoja, amesema kilichomuondoa ni
maslahi na hakuwa na jinsi.
“Mwadui
wamenipa dau zuri zaidi ya lile la Mbeya City. Mpira ndiyo kazi yangu, hivyo
naangalia maslahi na si kingine,” alisema Nonga.
Ikumbukwe kuwa
dirisha la usajili bado halijafunguliwa na kuna uwezekano wa wachezaji zaidi
kuihama timu hiyo ambayo nayo imewasajili Gideon Brown aliyetokea Ndanda,
Haruna Shamte (JKT Ruvu) na Joseph Mahundi (Coastal Union).
0 COMMENTS:
Post a Comment